KAMA UMEPENDA BLOG HII UNAWEZA KULIKE PAGE YETU KWA TARIFA ZAIDI

Majina ya kusisimua ambayo watu wamewahi kupewa duniani

 
Majina ya kusisimua ambayo watu wamewahi kupewa duniani Ushawahi kusikia majina yenye kusisimua? Bila shaka umekutana nayo mengi katika jamii yako. Kwa mfano, katika jamii ya Kitanzania tumekwishakutana na majina kama Kibakuli, Siogopi, Sinataabu ama hata Ngonjera. Kwingineko duniani, hali ni ile ile. Yafuatayo ni majina ya kusisimua ambayo watu wamewahi kupewa duniani.
 1. Canaan Banana Canaan Banana alikuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe huru Waziri Mkuu wake akiwa Robert Gabriel Mugabe. Alikuwa mhubiri wa Kimethodisti. Aliondolewa madarakani 1987. Alifariki 2003

 2. Praise-God Barebone Praise-God Barebone alikuwa muuza ngozi na mhubiri wa Kiingereza. Alichaguliwa kwenye Bunge la jamhuri ya Uingereza mwaka 1653. Alifariki 1679.

3. Walter Russell Brain Baron Brain alikuwa mtaalamu wa ubongo. Aliandika kitabu kuhusiana na magonjwa ya ubongo “Brain’s Diseases of the Nervous System”, pia akawa mhariri wa muda mrefu sana wa jarida la kitabibu liitwalo, Brain. Alipewa heshima ya kifalme mwaka 1952 akaitwa Baron Brain,1962. Alifariki 1966.

 4. Marc Breedlove Marc Breedlove ni profesa wa Neuroscience Chuo Kikuu cha Michigan State. Anajulikana zaidi kwa utaalamu wake kuhusiana na mambo ya kujamiiana na tabia zake.

 5. Thursday October Christian Thursday October Christian mtoto wa kwanza wa Fletcher Christian (kiongozi wa uasi wa Bounty) na mkewe Maimiti kutoka Tahiti. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 14 Oktoba, alipewa jina hilo kwa kuwa Fletcher Christian hakutaka kumpa mwanawe jina litakalomkumbusha Uingereza. Thursday alifariki mwaka 1831.

6. Thomas Crapper Crapper alikuwa fundi bomba wa Kingereza anayefahamika zaidi kwa kubuni vyoo vya kuflashi. Alifariki mwaka 1910.

 7. Prince Octopus Dzanie Prince Octopus ni bondia wa ngumi za ridhaa kutoka Ghana aliyeshiriki Summer Olympics mwaka 2008 na michezo ya Madola 2006.

 8. Argelico Fucks Fucks ni mcheza kandanda wa Brazil.

 9. Learned Hand Learned Hand jaji wa Kimarekani na mwanafalsafa wa mambo ya sheria. Alifariki mwaka 1961.

10. Ima Hogg Ima Hogg, maarufu kama “The First Lady of Texas”, mmoja wa wanawake wanaoheshimika zaidi kwenye jimbo la Texas katika karne ya 20. Alipigania sana kuondoka kigezo cha rangi na jinsia katika elimu. Alifariki 1975.

11. Rusty Kuntz Kuntz mchezaji wa zamani katika Ligi ya Baseball. Sasa ni kocha wa Kansas City Royals.

 12. Chuck Long Chuck Long is the head football coach at San Diego State University. He played quarterback in college at the University of Iowa and professionally with the Detroit Lions and the Los Angeles Rams. He is an inductee of the College Football Hall of Fame.

13. Adolf Lu Hitler Marak Adolf Lu Hitler R. Marak ni mwanasiasa wa Meghalaya, India. Jina lake si la ajabu huko Meghalaya, ambako wanasiasa wengine wamepewa majina kama Lenin R. Marak, Stalin L. Nangmin, Frankenstein W. Momin, ama Tony Curtis Lyngdoh. Hitler Marak aliliambia gazeti la Hindustan Times: “Pengine wazazi wangu walilipenda jina na wakanibatiza mimi Hitler....ninalifurahia jina langu, ingawa sina chembechembe zozote za udikteta."

14. Ten Million Ten Million alikuwa mchezaji wa baseball na amechezea timu kadhaa katika ligi ya Northwestern katika miaka kuelekea vita ya kwanza ya dunia. Alikuwa maarufu sana kutokana na jina lake. Alifariki mwaka 1964


15. Chris Moneymaker Chris Moneymaker ni mchezaji wa poka na ameshiriki katika World Series of Poker mwaka 2003.

16. Revilo Oliver Revilo Oliver alikuwa profesa wa filolojia, Kispaniola, na Kitaliano wa Kimarekani kwenye chuo kikuu cha Illinois. Alifariki mwaka 1994.

17. Richard Plantagenet Campbell Temple-Nugent-Brydges-Chandos-Grenville Richard Plantagenet Campbell Temple-Nugent-Brydges-Chandos-Grenville alikuwa kiongozi wa Uingereza na rafiki wa karibu sana wa Benjamin Disraeli. Alifariki mwaka 1889.

18. Peerless Price Peerless Price ni wakala wa mpira wa miguu wa Kimarekani.

19. Jaime Sin Jaime Sin alikuwa askofu wa Kifilipino bishop ambaye baadaye alikuwa Askofu Mkuu wa Kikatoliki huko Ufilipino na baadaye kuwa Kardinali Sin. Alifariki mwaka 2005.

 20. Wolfgang Wolf Wolfgang Wolf ni kocha wa kandanda wa Kijerumani ambaye pia amewahi kuifundisha Wolfsburg FC. Imeandikwa naJames kuzwa.

0 comments:

Post a Comment